BREAKING NEWS

Download

Saturday, September 4, 2010

Young Deeee tena on Ubungo plaza

Roma Atoa Onyo kwa Vyama vya Upinzani


Rapper katika Game ya Bongo flava Roma Mkatoliki, amevishukia vyama vya Upinzani vinavyotumia ngoma zake za Pastor na Tanzania katika kampeni zao za kisiasa bila ruhusa yake.


Roma amesema amewahi kushuhudia moja wapo ya Kampeni ya kisiasa ikitumia nyimbo zake na amevionya vyama hivyo kuacha mara moja, au wamfuate kuongea nae ili waelewane kibiashara.
Roma amesema ametoa muda kwa Vyama vya siasa vya Upinzani vinavyotumia ngoma zake katika mikutano yao na kampeni kumfuta ama kuacha kutumia, la sivyo atachukua hatua kali za kisheria dhidi ya wahusika hao, kwani wao wananufaika kwa kuwavuta mashabiki kwa kivuli cha nyimbo zake.

"Takers" yashika nafasi ya pili kwa mauzo Box Office


Movie ya Takers imeingiza dola milioni 21 katika duka maarufu la filamu la BOX OFFICE, na imeshika nafasi ya pili ikiongozwa na filamu ya The Last Exorcism. Katika Action movie hiyo starring ni T.I, Chriss Brown, Idris Elba, imeshika nafasi ya pili kwa mauzo weekend iliyopita, muda mfupi tu baada ya kutoka.

The Washington Post linaripoti kuwa, Takers imeshindwa kwa point chache na movie ya kutisha ya The Last Exorcism ambayo imengiza dola milioni 21.3 wakati Takers imeingiza dola milioni 21 kamili.

Mafaniio hayo ya Takers yata boost mapato ya mwaka ya T.I ambayo yamefikia dola milioni 9, katika Movie hiyo T.I ni mhusika mkuu pia ameshiriki kwenye kuproduce.

Takers na The Last Exorcism, nzilifuatiwa na Movie nyingine kali inayoitwa The Expendables ambayo imengiza kiasi cha dola milioni tisa katika duka Box Office.
 
Back To Top
Copyright © 2014 Kato Kumbi. Designed by OddThemes