BREAKING NEWS

Download

Saturday, September 4, 2010

Roma Atoa Onyo kwa Vyama vya Upinzani


Rapper katika Game ya Bongo flava Roma Mkatoliki, amevishukia vyama vya Upinzani vinavyotumia ngoma zake za Pastor na Tanzania katika kampeni zao za kisiasa bila ruhusa yake.


Roma amesema amewahi kushuhudia moja wapo ya Kampeni ya kisiasa ikitumia nyimbo zake na amevionya vyama hivyo kuacha mara moja, au wamfuate kuongea nae ili waelewane kibiashara.
Roma amesema ametoa muda kwa Vyama vya siasa vya Upinzani vinavyotumia ngoma zake katika mikutano yao na kampeni kumfuta ama kuacha kutumia, la sivyo atachukua hatua kali za kisheria dhidi ya wahusika hao, kwani wao wananufaika kwa kuwavuta mashabiki kwa kivuli cha nyimbo zake.

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 Kato Kumbi. Designed by OddThemes