BREAKING NEWS

Download

Saturday, September 11, 2010

WITNESZ AANDAA BATA PARTY


Female Mc Witnesz ameandaa Party ya kusherehekea Kuteuliwa katika tuzo za Channel O music Video Awards, Party hiyo inatarajiwa kuhudhuriwa na Celebrities kibao kutoka sehemu mbalimbali za Bongo na nchi za Jirani. Witnesz anasema ameamua kuweka kiingilio katika siku hiyo ili kuepusha utitiri wa watu kwani ukumbi huo unaweza kuelemewa hali ambayo inaweza kusababisha vurugu.

Katika Party hiyo kutakuwa na sehemu ya VIP ambayo ameipa jina la Bata, sehemu ambayo washakaji zake wa karibu ndo watakua wamechill.

Kiingilio katika Party ni kidogo, 5000/= ukinunua tiketi kabla na mlangoni siku ya tukio itakua shilingi 10,000/= Party hiyo itafanyika katika Ukumbi wa Buddha blu, Victoria karibu na Hospitali ya Kairuki.

Ili kumpigia kura Witnesz aweze kunyakua tuzo za Channel O Music Videoz Awards ingia kwenye mtandao wa Channel O Music video Awards utaweza kupiga kumpigia kura au tuma msg kupitia simu yako ya mkononi, andika: 1B kwenda namba +27 83 920 8406

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 Kato Kumbi. Designed by OddThemes