BREAKING NEWS

Download

Tuesday, September 7, 2010

BAADA YA KUTENGENEZA MKWANJA MREFU GODZILLA AAMUA KUWASAIDIA WASANII WACHANGA



Rapper Godzilla a.k.a The Sala sala President ameamua kuanzisha Label yake na kuipa jina la Godzilla Inc, Alipozungumza na 255 Godzilla amesema kuwa hatua hiyo inatokana na kupiga mkwanja mrefu(milioni tano) wakati wa Tour zake alizofanya kuanzia mwezi wa kwanza mwaka huu mpaka mwezi wa nane 2010, lakini pia sababu nyingine ni kutokana na kuona vipaji vingi vikizagaa mtaani na kupotea kabisa hali ambayo inahatarisha Game ya bongo flava siku za Usoni.

Zilla anasema anaendelea kupokea wasanii wanao weza game na hana idadi maalium anachotaka yeye ni kusaidia vipaji vipya. Tayari Godzilla Inc imeshaanza kufanya kazi na wasanii wawili ambao wamerekodi katika studio tofauti za jijini Dar es salaam.

Kwa hiyo kama wewe unajiamini ni mkali na bado haujatoka, mcheki Godzilla pande za salasala atakuskiliza na kukupa Yes Or No, ukipata Yes basi ndo safari yako ya kimuziki itakua imeanza vizuri kabisa.

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 Kato Kumbi. Designed by OddThemes