BREAKING NEWS

Download

Tuesday, July 30, 2013

The Session - Mswaki HD

Behind The Scene In The Making of Country wiz ft Gnako -Watch me

Behind the Scenes Of Mwambie Mwenzio : Stamina ft Darasa and Warda




New Music : Uprise music : Leo ft Quick Rocka & Slim Sal -No Silence

New Music : De Fatality 2013 Presents : Country wiz ft Gnako -Watch Me Prod.Mesen Selekta

               COUNTRY WIZ FT GNAKO -WATCH ME
Official Release : DOWNLOAD HAPA
Produced by Mesen Selekta ..
DEFATALITY MUSIC 2013

New Music : Stamina Feat Darasa and Warda -Mwambie mwenzio

Song:Mwambie Mwenzio
Artists:Stamina ft Darasa&Warda
Studio:One Love Fx
Producer:Tiddy Hotter
Song writers;sStamina(verses)Darasa(choruss)
Intro:(stamina)
stamina)……you what tiddy?this is one love fx,shorwebwenzi on this one,itc moro town beiiib

vers 1(stamina)
wakuja rudi bushi,mji unahitaji waliosoma.
Kicheche usikae uchi,huku umevaa sketi ya ngoma.
Safisha kope,braza mungu sio deusi.
We hushangai mzungu mweupe,ila ana kivuli cheusi.
Kuitwa lijali,ina maana nyumbani tule.
Ukimwi kuutibu aghali,sasa iweje uupate kwa bure.
Binti usitoe mimba,ukihisi utakosa soko.
Zaa umtunze kinda,mbinguni usichomwe moto.
Acha kuiba,we fisadi uliyetukuka.
Mstue na ngariba,nae aache watu wanakufa.
Dogo unayekunywa gongo,ukifa utazikwa la mboto.
Na denti skuli ndo mchongo,ya mjomba mwachie mpoto.
Teja pandisha mlege,rudisha kete kwa pusha.
Mwambie atanyea debe,akikamatwa na vya arusha.
Acha makuzi,mpendaji ili ufike mbali.
Mapenzi king’amuzi,na pesa ndo digitali.

Choruss (darassa&warda)
Vipi umekaa, chini,na muda unakwenda mbio./
Kwenye nchi masikini,na wingi wa matukio./
Waambie jamaa,huu ni mwendelezo sio ujio./
Niko na kitu cha kusema,nipe muda na sikio./
Ukiwa mtaani,hizi ripoti(mwambie mwenzio)
Au umechill masikani jirani(mwambie mwenzio)
Mfanyakazi au mkulima shambani(mwambie mwenzio)
Mwanafunzi na mitaa huu ujumbe(mwambie mwenzio)

Vers 2(Stamina)
Ewe mtegemea ndugu,mwenye mikono na miguu.
Umasikini tatizo sugu,kuliko hata mr II.
Baba la baba,weka ubaba kila level.
Kitaani usawa unakaba,hadi padri anaishi kwa devil.
Mabadiliko,daima huanza na wewe.
Kama unakokwenda siko,uliza ili usichelewe.
Mche mungu,kama hajapanga hajapanga.
Kama ridhiki mafungu,kwanini ushinde kwa mganga.
Kusoma mpaka uchizi,ni kukosa kujiamini.
Mvivu unayependa usingizi,utakufa ukiwa masikini.
Endapo utailaza akili,usitegemee shida kukuamsha.
Hakuna mpenzi kama dili,funga nae pingu za maisha.
Hakuna tofauti,kati ya tajiri na masikini.
Uvae bukta uvae suti,ila wote tutazikwa chini.
Msimtenge mkiwa,kisa wazazi wake walimtupa.
Hata ng’ombe ana maziwa,ila akila simu anakufa.

Choruss (darassa&warda)
Vipi umekaa, chini,na muda unakwenda mbio./
Kwenye nchi masikini,na wingi wa matukio./
Waambie jamaa,huu ni mwendelezo sio ujio./
Niko na kitu cha kusema,nipe muda na sikio./
Ukiwa mtaani,hizi ripoti(mwambie mwenzio)
Au umechill masikani jirani(mwambie mwenzio)
Mfanyakazi au mkulima shambani(mwambie mwenzio)
Mwanafunzi na mitaa huu ujumbe(mwambie mwenzio)

Vers 3(Stamina)
Huna hata cheti cha form 4,na una ndoto za kuwa raisi.
Nyumbani unajaza choo,hupaswi kungoja na urithi.
Kufeli hasara,akili hailetwi na milo.
Sio kisa dunia duara,ndo denti upate ziro.
Kila kitu kizuri,duniani huletwa na pesa.
Kwanza elimu haina umri,usiogope kusoma memkwa.
Ujanja hauna miaka,kiujinga we baki mdogo.
Acha uchu wa madaraka,kwa kuongoza hadi vigogo.
Hivi vifo vya wasanii,vinatokea kama ajali.
Ee mungu mshushe nabii,atukumbushe kusali.
Tumia akili,maishani uongoze jahazi.
Na usitafute utajiri,kwa kumtoa kafara mzazi.
hujachelewa bado,cha msingi we piga kago.
Shukuru bado unahema,wala usishushe vilago.
Kijana taifa la leo,usilale ijenge kesho.
Huu ukoloni mambo leo,usikufanye ujione special.

Choruss (darassa&warda)
Vipi umekaa, chini,na muda unakwenda mbio./
Kwenye nchi masikini,na wingi wa matukio./
Waambie jamaa,huu ni mwendelezo sio ujio./
Niko na kitu cha kusema,nipe muda na sikio./
Ukiwa mtaani,hizi ripoti(mwambie mwenzio)
Au umechill masikani jirani(mwambie mwenzio)
Mfanyakazi au mkulima shambani(mwambie mwenzio)
Mwanafunzi na mitaa huu ujumbe(mwambie mwenzio)

Outro(warda)
Mwambie mwenzio (mwambie mwenzio)x4

New Music : Janjaro- Serebuka Ft.Jambo Squard Prod.Dx Noizmekah

Dogo Janja aka Janjaro Feat Jambo Squad 
SEREBUKA 

HotJerry :Best Of The Best Interview 3 with Leo

Kama kawaidaaaaaaaaaa Best Of The Best Interviews Zinaendelea ..Chini ya Yule Presenter wako Mkaliii HotJerry Na HII NI Interview ya Tatu tukiwa na Leo 'Mysterio' Wack Member aliewahi kuwa Bhits sambamba na MABESTE IDAKE HAPA CHAP  
DOWNLOAD HAPA
Pia atatambulisha ngoma yake mpya Akiwa na Quick Racker pamoja na sLIMsAL NO SILENCE
 
 
Back To Top
Copyright © 2014 Kato Kumbi. Designed by OddThemes