BREAKING NEWS

Download

Wednesday, August 1, 2012

Gentriez Atoa Tamko Kuhusiana na Tetesi za Kugombewa Na Studio


Baada ya Kujawa kwa Tetesi Kuhusiana Na Studio za Mjini ARusha kumgombea Msanii kutoka River Camp Soldiers anayejulikana kama Gentriez Mwakitabu na Pande zote mbili ziliongea na Mtandao wa Nolniz Blog kupitia Reporters wake Abdullaziz na Nolniz mwenyewe na Haya Ndio yalikua moja ya mazungumzo na WANENE C.E.O Darsh Pandit
"Upande wake CEO wa Wanene entertainment Darsh Pandit
amesema hakuna tatizo lolote wala kutoelewana kokote kule kati yake yeye na Nisher kwani kweli Gentriez alikuwa kijana wake muda mrefu kabla yeye hajaenda masomoni nje na aliporudi amemkuta akifanya kazi na Nisher na haoni kama ni jambo baya kwani amesikiliza vitu vilivyofanyika na ameona ni kazi zinazoeleweka na zipo njema..!!"
Upande wake Nisher yeye amesema Gentriez ni Msanii wake, amefanya naye kazi za kutosha na ndiye aliyemtoa, hivyo Gentriez yupo chini ya Label yake ya Nisher Entertaiment

.Maelezo kwa Hisani ya NOLnIZ BLOGSPOT

Baada ya Muda kidogo baada ya kuvuma kwa hio tetesi Gentriez Mwenyewe aliweka wazi Maelezo yake yeye kama MSANIII HUSIKA wa Tukio Hilo katika Mtandao wa Kijamii wa Facebook na Huu Ni Uthibitisho wa GENTRIEZ MWAKITABU Aliouweka Facebook


Maneno yakisomeka
"Hii ndio contract/mkataba wangu niliosaini kuwa msanii wa record lebel ya wanene entertainment.. napenda watu watambue hilo kuwa nipo chini ya record lebel ya wanene entertainment... Sina mkataba na record lebel nyngne yeyote kama inavyosema wala siko nako to nako wala weusi mimi ni mriver camp,.. Asanteni sana and wanene in the house"
Pia Akiandamisha na Picha akiwa na C.E.O Darsh Pandit

Taarifa za Mahojiano zimefanyika chini ya Blog ya Norlens Ijulikanayo kama Nolniz ya ARUSHA TZ

Share this:

Post a Comment

 
Back To Top
Copyright © 2014 Kato Kumbi. Designed by OddThemes